• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Kwa kuangalia *TV* live kwa kutumia *Simu*ikiwemo *AZAM, CLOUD, TBC* na za *michezo kibao*, bonyeza hii *link* hapa chini, na kui *download*
http://www.jamiiforums.com/attachments/online-tv-apk.423158/
Share:

Rwanda yashtumiwa kupanga shambulizi la kutaka kumuua msaidizi wa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Rwanda yashtumiwa kupanga shambulizi la kutaka kumuua msaidizi wa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Nchi ya Burundi imeishutumu Rwanda kwa madai ya kupanga kufanya majaribio ya kutaka kumuua msaidizi wa Rais Pierre Nkurunziza, Willy Nyamitwe.

Msemaji wa jeshi la polisi kutoka Burundi, Pierre Nkurukiye amesema maagizo ya kufanywa kwa jaribio hilo lililofeli, yalitumwa kutoka nchini Rwanda kwa wapangaji waliotoka kwenye jeshi la Burundi.

Nyamitwe alivamiwa alipokuwa akirudi nyumbani mwake Magharibi mwa Kajaga huko Burundi lakini si mara ya kwanza kupatwa na tukio kama hilo. 

Mwezi Julai mwaka huu Burundi iliishtumu Rwanda kwa mauaji ya Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Hafsa Mossi aliyeuawa kwa kupigwa risasi mjini Bujumbura.

Share:

Chadema: Hatutakubali tena kudhulumiwa 2020

Chadema: Hatutakubali tena kudhulumiwa 2020

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) ,Vincent Mashinji amesema hawatakubali tena kudhulumiwa kwa namna yoyote  katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Dk. Mashinji amesema hayo huku akimtolea mfano wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, na kuongeza kuwa kuna mambo hutokea bila kutarajia lakini watapambana kwa kila hali,

“Huu ni uchaguzi kuna mtu alitarajia haya yaliyofanywa na Jecha? hii inaonyesha kwenye nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki, wewe umefanya mara ya kwanza tukanyamaza,ukafanya tena mara ya pili kibabe,tukalalamika, badala ya kutuita tuongee, unasema nendeni mkaseme kokote kule”alisema Mashinji.

Aidha, akiongelea utawala wa Rais Magufuli ,Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utawala bora na matokeo yake yeye ndio amekuwa kila kitu, ameongeza kuwa wakati anaanza  mapambano na rushwa aliamini kwamba angeweza kuliondoa tatizo hilo lakini imekuwa tofauti.

Hata hivyo, Mashinji ameongeza kuwa katika mwaka mmoja wa Rais Magufuli, amesema ameshindwa kusimamia utawala bora baada ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja na shughuli zote za kisiasa nchini kwa kile alichosema kuwa muda wa siasa umekwisha.

Share:

RC Paul Makonda Atuhumiwa Kuwadhalilisha Watumishi wa Umma kwa Kuwaita VICHAA........Tazama Video

RC Paul Makonda Atuhumiwa Kuwadhalilisha Watumishi wa Umma kwa Kuwaita VICHAA........Tazama Video


KAULI mbalimbali zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa ziara zake zimezua taharuki jijini humo.

Kwa nyakati mbalimbali wakati wa ziara zake,  Makonda anadaiwa kutoa kauli za vitisho hasa kwa watumishi wa umma.

Kutokana na hali hiyo, Chama cha ACT-Wazalendo kimemshtaki mkuu huyo wa mkoa katika Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Utawala Bora ili imuwajibishe.

Katika taarifa yake iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Katibu wa Ngome ya Wanawake wa chama hicho, Esther Kyamba alisema kauli alizozitoa Makonda zimewadhalilisha watumishi hao.

“Tumesikitishwa na kuhuzunishwa na kauli zisizo za kiuongozi na zisizozingatia kanuni za maadili ya utumishi wa umma zinazoendelea kutolewa na RC Makonda.

“Jana (juzi), katika mkutano anaouita wa kutatua kero kwa wakazi wa Dar es Salaam aliendelea kushindwa kutatua kero na badala yake kuongeza kero ya kudhihaki, kudhalilisha kukejeli na kutukana hadharani wananchi anaowaongoza na watumishi anaowasimamia kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya Watanzania,” alisema.

Kyamba alisema kitendo cha Makonda kumtolea lugha ya udhalilishaji Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni, Rehema Mwinuka akiwa Mabwepande kwa kumtamkia kwamba “Hawa ndio vichaa tunaohangaika nao, toka hapa”. Hakikubaliki.

“Kauli hiyo imetushtua sana,tunalaani kwa nguvu zetu zote, kauli kama hii si tu haikupaswa kutolewa na kiongozi mkubwa katika ngazi ya mkoa lakini pia ni kauli mbaya ambayo ililenga kumdhalilisha Rehema na kumvunjia heshima yake mbele ya umma,” alisisitiza.

Alisema kutokana na udhalilishaji huo uliofanywa na Makonda, wameshawasilisha mashtaka yao dhidi yake mbele ya Tume, wakiitaka imwajibishe kwa kitendo chake hicho cha utovu wa nidhamu na maadili ya utumishi wa umma.

“Ngome inamtaka mkuu huyo wa mkoa kutambua kuwa kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 pamoja na Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma, kanuni ya 65(1) inamtaka mtumishi wa umma, “kuepuka kufanya vitendo viovu au kutamka maneno yanayolenga kuwaaibisha watumishi wa ngazi moja, za chini yao au wa vyeo vya juu,” alisema.

Alisema kitendo alichofanya, kumwaibisha na kumtolea lugha ya udhalilishaji, Mwinuka ni kinyume cha Sheria na Kanuni za Utendaji katika Utumishi wa Umma.

“Tunaitaka Tume ifanye uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya matamshi mbalimbali yaliyotolewa na Makonda ambayo yalikiuka sheria ya Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma.

“Tunayataka mashirika na asasi mbalimbali zinazosimamia haki za binadamu, haki za jinsia na utawala bora kupaza sauti dhidi ya kauli isiyo ya kiuongozi ya  Makonda, Ngome na Chama kwa ujumla tutaendelea kuwasemea wanyonge wote popote walipo kwa kadri ya uwezo wetu,” alisema.
Share:

Selfie ya Diamond akiwa na BOXER Yazua Balaa Mitandaoni

Selfie ya Diamond akiwa na BOXER Yazua Balaa Mitandaoni

Diamond Platnumz amezua balaa mtandaoni baada ya Jumanne hii kupost selfie akiwa amevalia kiboxer cheusi.

Kwenye picha hiyo, Diamond aliandika: Straight from the Changing room!…I think i need to go back to the gym so that i can be more flexible on m 24th Pre-XMass Parformance in Dar Es Salaam.

Licha ya kufunika kwa emoji kwenye eneo la sehemu zake za siri, selfie hiyo imesababisha hisia tofauti huku wengi wakimponda staa huyo kwa kukosa staha.

Hizi ni baadhi ya comments:

isaac_siame: @diamondplatnumz sitaki kuamini kama mawaziri kama nape au makamba watatamani kuja tena wcb kuonana namsanii wa namna hii, hii itakucost au imekucost tayari @babutale busara zako azijatumika kushauri hii naanza kuona misingi ya heshima ulioitunza kwa mda mrefu ikipotea

tausizehemasaleh: You ‘ve a beautiful soul but I think sometimes you go over board,remember to much is given .much is expected,I respect the path Mom Tee is taking,don’t neglect her advices,you may need them sometimes,Big love small bro

yahyakiwera8646: Nduguyangu nakuusia usidanganyike nahizi like nacomment kumbuka weweni muislamu nautazikwa kiislamu kuogope mungu kwanza niharamuvhizo tatoo ukiswali swalazako haziswihii ukiogajanaba halitoki nduguyangu unapotea HAWA wanao like wote kaburini hatakuwepo utakua pekeyako namatendoyako iwemazuri au mabaya je utaponaa? Ilahuu WANGU niukumbushotu kwako nikutakie mabadiliko usijekusema hukuambiwa buree miminisha kuambia

swaum1140: Mmmm jaman mm hapo hapan nasibu sio nzuri hyo pic kwa kweli kumbuka wew ni baba now sio pich nzur kumbuka IPO cku tifa ataiona alaf itakua aibu kubwa uxifany hvy bhana hapo mm sijapenda kabisaaa

ommie_latino26: Bro huo ni ujinga una familia sasa ina maana hapo tiffah aje aone dudu ya baba au

Share:

Uongozi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote waeleza sababu ya kusitisha uzalishaji

Uongozi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote waeleza sababu ya kusitisha uzalishaji


UZALISHAJI katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara umesimama kwa muda kutokana na hitilafu za kiufundi zilizojitokeza katika mitambo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Tanzania, Harpreet Duggal alisema jana kwamba mafundi wa Dangote wapo kazini na shughuli za uzalishaji zitarejea katika siku chache zijazo.

Alisema kiwanda kinachomilikiwa na bilionea namba moja Afrika, Alhaji Aliko Dangote wa Nigeria kilianza uzalishaji wa kibiashara mwaka huu na kama ilivyo kwa kiwanda kingine kama hicho, jambo lolote linaweza kutarajiwa hasa katika miezi ya mwanzo.

Alisisitiza, “hitilafu hizi ni za kawaida na uzalishaji utarejea katika kipindi kifupi kijacho.”

Akizungumzia gharama za uzalishaji, Duggal alisema uendeshaji nchini uko juu huku miongoni mwa sababu ikiwa ni matumizi ya jenereta za dizeli katika kuendesha kiwanda.

Hata hivyo, alisema serikali inaangalia suala hili la gharama na jinsi ya kutafuta njia ya kuwapunguzia mzigo.


Share:

VIDEO: Masikilize Rais Magufuli Akipiga Marufuku Watu Binafsi Kuuza Sare za Majeshi

VIDEO: Masikilize Rais Magufuli Akipiga Marufuku Watu Binafsi Kuuza Sare za Majeshi


Rais Magufuli akizungumza na watumishi wa gereza la ukonga alipotembelea kwa kushtukiza jana. Kapiga marufuku watu binafsi kuuza sare za majeshi
Share:

Makada Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Wazuru Tanzania Kujifunza toka CCM

Makada Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Wazuru Tanzania Kujifunza toka CCM

UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uko nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli zinazofanywa na CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama hicho, Jia Bo.

Madabida alisema lengo la ziara hiyo ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China ulioasisiwa na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Baba wa Taifa la China, marehemu Mao Tse-Tung.

Alisema ujumbe huo ambao utatembelea Temeke na Zanzibar uliwasili nchini baada ya ziara ya baadhi ya makada wa CCM waliokwenda China na kujifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.

Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Dk Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.

"Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi zingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba na zinginje za  Ulaya hasa katika siasa za kijamaa," alisema Chana.

Alisema China wako karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyopiga..
Share:

Video mpya ya Navy Kenzo – Feel Good Ft. Wildad (Official Music Video)

Video mpya ya Navy Kenzo – Feel Good Ft. Wildad (Official Music Video)

Kundi la muziki kutoka nchini Tanzania, Navy Kenzo linaloundwa na wasanii wawili Aika na NahReel jana Novemba 29 wameachia video ya wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la Feel Good. Itazame video hiyo hapa chini.
 

Share:

Waziri Mkuu aziagiza shule na majeshi kuachana na kuni.........Waziri Maghembe Aahidi Kupandisha Kodi ya Mkaa Maradufu

Waziri Mkuu aziagiza shule na majeshi kuachana na kuni.........Waziri Maghembe Aahidi Kupandisha Kodi ya Mkaa Maradufu

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za serikali zinazotumia kuni na mkaa kwa wingi kama vile shule na majeshi kuanza mikakati madhubuti ya kubadili mfumo wa kupikia na kuweka majiko ya gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa ambayo yamekuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.

Alisema hayo jana Dar es Salaam katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kujadili namna na njia bora ya kupunguza matumizi ya mkaa kwa usimamizi endelevu wa mazingira nchini.

“Nimeelezwa kuwa makampuni yanayouza majiko na gesi ya kupikia aina ya LPG yameonesha nia ya kuweka majiko haya bila gharama yoyote. Tutumie vyombo vyetu vya habari na majukwaa ya mikutano kuhamasisha wananchi kutumia fursa hii ya LPG,” alisema Waziri Mkuu.

Aidha, alisema nchi inakabiliwa na changamoto kubwa za uharibifu wa mazingira kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ufugaji wa kuhamahama, mifugo kuvamia misitu na kuiharibu pamoja na vyanzo vya maji na watu kukata miti katika vyanzo hivyo.

Alisema mabadiliko ya tabianchi yamesababisha mabadiliko ya vipindi vya mvua, mtawanyiko wa kiwango cha mvua na hivyo kutishia usalama wa chakula na ukosefu wa malighafi kwa viwanda ambavyo ndiyo njia ya kuivusha nchi kuingia katika uchumi wa kati.

Alisema takwimu zinaonesha asilimia 90 ya nishati ya kupikia hasa mijini ni mkaa na kwa vijijini asilimia kubwa na wananchi wanatumia kuni ambapo takwimu hizo pia zinaonesha ili kuzalisha tani moja ya mkaa sawa na magunia 30 zinahitajika tani 12 za kuni na hali hiyo imesababisha nchi kupoteza zaidi ya hekta 370,000 kila mwaka.

Alisema utafiti pia umebainisha kwamba matumizi ya mkaa yanaongezeka kutokana na ongezeko la watu na kama haitaanza kutumika nishati mbadala, mahitaji ya mkaa yatafikia takribani tani milioni tano kwa mwaka ifikapo mwaka 2030 kutoka tani milioni 2.4 zilizotumika mwaka 2015.

Hata hivyo, Profesa Maghembe alisema wizara yake inatarajia kupandisha ushuru na kodi ya mkaa ili uuzwe kwa bei ya juu lengo likiwa ni kuwafanya wasafirishaji na wanunuzi washindwe kumudu gharama na hatimaye matumizi ya mkaa kupungua.
Share:

Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Askari wake Aliyefariki Dunia Kwa Kujipiga Risasi

Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Askari wake Aliyefariki Dunia Kwa Kujipiga Risasi

Jeshi la Polisi mkoani Pwani limezungumzia kifo cha askari wake PC Armand Furaha (33) aliyejipiga risasi kifuani bila kukusudia na kufariki dunia.

Askari huyo alijipiga risasi hiyo usiku akiwa anaelekea kwenye lindo nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.

Tulio hilo lilitokea saa moja usiku eneo la Mailimoja sokoni usiku wa kuamkia jana, wakati askari huyo akiwa njiani kuelekea kwenye kituo cha lindo alichopangiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Pwani, Blasius Chatanda amesema askari huyo alijipiga risasi bahati mbaya kwa bunduki aina ya SMG akiwa amekaa kwenye kiti cha mbele katika gari alilokuwa anasafiria kwenda lindoni.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa askari huyo alikuwa tayari ameweka risasi chemba kwenye bunduki hiyo aliyokuwa nayo na kwa bahati mbaya akiwa anashuka kwenye hilo gari ndipo risasi hiyo ikafyatuka na kumpiga kifuani eneo la kushoto na kufa wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tumbi.

“Kabla ya tukio hilo, askari huyu aliwasili kazini jioni na kukuta amepangiwa kituo cha ulinzi kwa mkuu wa wilaya hivyo kama ilivyo ada alichukua zana za kazi ikiwemo bunduki hiyo na kuanza safari ya kuelekea lindoni kwake huko kwa DC, lakini bahati mbaya hakufika alifariki kwa kujipiga risasi bahati mbaya,” amesema Chatanda.

Akizungumzia suala la askari kujipiga risasi Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema kila tukio hutokana na mazingira tofauti.
Share:

UKIMWI sasa kudhibitiwa kwa njia ya simu

UKIMWI sasa kudhibitiwa kwa njia ya simu


Tanzania imeingia rasmi kwenye mfumo maalum wa kimataifa wa kupata huduma za afya ya UKIMWI kwa njia ya simu bila malipo mfumo ambao umefadhiliwa na nchi ya Marekani.

Akizindua mfumo huo Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Virginia Blaser amesema mfumo huo utawafikia zaidi ya watu laki nane huku lengo kuu la mfumo huo likiwa ni kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kutoka asilimia 7.5 mpaka asilimia 5 hadi kufikia asilimia 0.0.

Amesema watu wote ambao wanadhaniwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi hadi kufikia mwaka 2020 wawe tayari wamepimwa kwa asilimia 90, asilimia 90 waanze kutumia dawa, na asilimia 90 kiwango chao cha maambukizi kiwe kimepungua.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya TAYOA nchini Bw . Peter Masika amesema katika ufadhili wa mfumo huo wao wakiwa ni wasimamizi wa mfumo watahakikisha unawafikia watanzania wote hasa wale wasiofikiwa na huduma muhimu za kiafya na kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutumia mfumo huo ili kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi.

Share:

Pedeshee Ndama mtoto wa Ng’ombe Kortini kwa Kutakatisha Hela

Pedeshee Ndama mtoto wa Ng’ombe Kortini kwa Kutakatisha Hela

Tuhuma za kughushi, kutakatisha fedha na kujipatia dola za Marekani 540,390 kwa njia ya udanganyifu zimemfanya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Ndama Shabani Hussein, maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto wa Ng’ombe (44) kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mashtaka hayo yanaangukia katika Sheria ya uhujumu uchumi.

Akisoma hati ya mashtaka jana Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa mshtakiwa huyo alifanya hivyo na kujipatia dola za Marekani 540,390 kwa njia ya udanganyifu kati ya Februari 26 na Machi 3,2014.

Msigwa amedai kuwa Februari 20,2014 jijini Dar es Salaam, Ndama alighushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 yakiwa na thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Machi 6,2014 katika jiji la Dar es Salaam, alighushi kwa kutengeneza hati ya kibali (Certificate of Clearance) ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam, akijaribu kuonesha kilogramu 207 za dhahabu toka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.

Wakili huyo wa Serikali ameendelea kudai kuwa Februari 20,2014 mshtakiwa huyo alighushi fomu ya forodha yenye namba za usajili R.28092 akionesha kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited imelipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) dola za Marekani 331,200 kama kodi ya uingizaji wa bidhaa ambazo zina uzito wa kilogramu 207 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000 kutoka Congo kitu ambacho si kweli.

Pia, mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa kati ya Februari 26 na Machi 2014 katika jiji la Dar es Salaam alijihusisha moja kwa moja na utakatishaji fedha kwa kufanya miammala ya dola za Marekani 540,390 kwa kuelekeza ziwekwe katika akaunti namba 9120000085152 iliyopo katika benki ya Stanbic yenye jina la Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited na kuzitoa taslimu wakati akijua fedha hizo zinatokana na zao la uhalifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi bado haujakamilika na mshtakiwa alipelekwa rumande kwa sababu shtaka la kutakatisha fedha linalomkabili ni miongoni mwa mashtaka yasiyo na dhamana.

Kesi imeahirishwa hadi Desemba 13,2016 kwa ajili ya kutajwa

Share:

Rais Lungu Akataa Biashara ya Uswahiba.....Ataka Ufanisi Zaidi Bandari ya Dar es Salaam

Rais Lungu Akataa Biashara ya Uswahiba.....Ataka Ufanisi Zaidi Bandari ya Dar es Salaam

Rais wa Zambia, Edgar Lungu amewataka watendaji wa nchi yake na Tanzania, kuweka siasa pembeni na kujikita kwenye biashara zitakazoinua uchumi wa nchi hizo mbili.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku tatu, Rais Lungu aliyetembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Kusafirisha na Kupokea Mizigo la Zambia (Zamcargo), alisema licha ya kuenzi mchango wa waasisi wa mataifa hayo, Mwalimu Julius Nyerere na Kenneth Kaunda, watajikita zaidi kwenye biashara.

 “Changamoto mliyonayo ni kwenu uongozi na Bodi ya TPA kwa watu wa Kusini au Mashariki au hata nje ya Afrika. Watu wa Zambia wanasema muda wa siasa umekwisha, sasa ni muda wa maendeleo. Hatutawaunga mkono kwa sababu niko karibu sana na Rais (John) Magufuli. Ni kweli niko karibu na Rais Magufuli kama mlikuwa hamjui, lakini hatuwaungi mkono kwa sababu hiyo, bali kwa ufanisi wenu,” alisema Rais Lungu.

Akizungumzia miradi ya reli ya Tazara na bomba la mafuta la Tazama, Rais Lungu alisema nayo inapaswa kufanya kazi kwa ufanisi.

 “Ni kweli sisi ni ndugu lakini hatuangalii hilo. Wazambia wanataka mbolea ifike haraka, shaba isafirishwe haraka kwenda sokoni,” alisema.

Akiwa katika ofisi za Zamcargo, Rais Lungu alirudia wito wake wa ufanisi wa biashara akisema hatasita kuwawajibisha watendaji wa taasisi hiyo.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko alisema Zambia  imekuwa mteja namba moja katika usafirishaji wa mizigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Kakoko alisema mwaka 2014, Zambia ilichangia asilimia 36 ya mizigo ambayo ni sawa na tani milioni 5.2 ikiwa ni mbali ya nchi nane zinazotumia bandari hiyo.

“Takwimu za TPA zinaonyesha kuwa mizigo ya Zambia inayopitia hapa imekuwa ikiendelea kila mwaka. Mwaka 2011, bandari ilipokea tani milioni 1.6 za mizigo inayotoka na kuingia. Lakini mwaka 2014 Zambia ilipokea tani milioni 1.9 za mizigo ya Zambia,” alisema Kakoko.

Alisema kutokana na umuhimu huo, uongozi wa TPA umekuwa ukiboresha huduma ili kufanya kazi kwa ufanisi.

“Kwa mfano, muda wa kutoa mizigo bandarini umepunguzwa hadi siku kumi na moja mwisho wa Oktoba kulinganisha na siku 32 zilizokuwa mwaka 2008. Bandari pia imeboresha mfumo wa malipo ya mizigo kwa wateja wake kwa kutumia mfumo wa kielektroniki,” alisema Kakoko.

Katika ziara hiyo ya bandarini, Lungu aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda, Balozi, Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani na katibu mkuu wa wizara hiyo, Dk Leonard Chamuriho.

Mara baada ya ziara hiyo Rais Magufuli aliwaongoza viongozi wengine wa Serikali kumsindikiza mgeni wake huyo uwanja wa ndege na kurejea Zambia.

Viongozi wengine waliofika uwanjani hapo ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine. Rais Lungu aliondoka uwanjani hapo saa 7: 40 mchana.
Share:

Ajali ya Gari Yaua Watu 6

Ajali ya Gari Yaua Watu 6

Watu  sita wakiwamo mfungwa na wanafunzi wamekufa huku wengine wanane wakijeruhiwa, baadhi yao vibaya baada ya gari dogo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka mara nne katika Kijiji cha Kipande wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa katika barabara kuu ya Mpanda – Sumbawanga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema ajali hiyo ilitokea saa 8.10 jana mchana katika Kijiji cha Kipande.

Aliwataja waliokufa kuwa ni mfungwa wa Gereza la Kitete lililopo Nkasi, Gaudensi Nyambo (27), Gasper Malimi (18) na Kenzi Mwambige (18) wote wakiwa wanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Nkasi na Ofisa Mipango wa Wilaya ya Nkasi, Godfrey Mwanansao.

Alisema marehemu wawili hawajatambuliwa huku miili yote ikiwa imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Rukwa ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga .

“Mfungwa Nyambo alikuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Kitete wilayani Nkasi ambako alikuwa na kesi nyingine mahakamani alikufa wakati akitibiwa hospitalini hapa,” alieleza Kamanda Kyando.

Alisema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Hiace Nissan Vannette lenye namba za usajili T 966 DHP lililokuwa likiendeshwa na Lusanjo Mwaipopo aliyekimbia baada ya ajali hiyo.

Alisema gari hilo lilikuwa likitokea wilayani Nkasi kwenda mjini Sumbawanga ambapo liliacha njia na kupinduka mara nne kabla halijaanguka ndani ya gema.

Alisema chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika huku uchunguzi wa kipolisi ukiendelea. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Dk John Lawi alisema majeruhi tisa wamepokewa hospitalini hapo ambao mmoja ambaye ni mfungwa alikufa OPD.

Aliwataja majeruhi kuwa ni pamoja na askari Magereza wa Gereza la Kitete, Fortunatus Saanane (44) aliyelazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU) huku hali yake ikiwa tete. Wengine ni askari Magereza, Francis Elay (30) ambaye alitibiwa na kuruhusiwa.

Kwa mujibu wa Dk Lawi, majeruhi wengine ni Mbagala Hale, Mamadelwa Kafadhila, Mathias Mwandaliwa (28) na wengine ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja. Alisema hali za majeruhi hao ni mbaya.

Share:

Mbunge Mwingine wa CHADEMA Atiwa Mbaroni

Mbunge Mwingine wa CHADEMA Atiwa Mbaroni

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke kwa tuhuma ambazo hazikuweza kujulikana mara moja.

Taarifa za kukamatwa kwa mbunge huyo, zilianza kusambaa  jana jioni, huku zikimuhusisha na mgogoro wa ardhi.

Katibu wa mbunge huyo, Deogratius Salit jana alikiri Waitara kukamatwa na polisi wakati wa ubomoaji wa nyumba za wakazi wa Kata ya Kivule.

Salit alisema nyumba hizo zilibomolewa baada ya kuwapo kwa mgogoro baina ya wananchi wa kata hiyo na Kikundi cha Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania (UVIKITA) kinachodaiwa kumili eneo hilo licha ya wananchi hao kushinda kesi mahakamani.

Alisema mbunge alifika kwenye eneo hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kwamba nyumba zao zinabomolewa na Jeshi la Polisi.

“Mbunge alifika katika eneo hilo baada ya kupata taarifa ya kuwapo kwa ubomoaji katika Kata ya Kivule na alifika pale kwa sababu yeye pia ni mwenyekiti wa kata hiyo.

“Baada ya kufika pale alikuta askari wakisimamia ubomoaji huku wakirusha mabomu ya machozi na kuwatawanya wananchi, aliwauliza askari kama wana nyaraka zozote za kuvunja nyumba hizo, ndipo walimwambia kuwa nyaraka hizo zipo kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Chang’ombe” alisema.

Salit alisema wakati wakiwa njiani kuelekea Polisi Chang’ombe, Waitara aliwataarifu kwamba amekamatwa na kupelekwa katika kituo hicho.

Alisema hadi sasa bado hawajajua sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo na wanamsubiri wakili wake aitwaye Hekima kwa mahojiano zaidi.

Salit alisema zaidi ya nyumba 200 zimebomelewa na kuwaacha wananchi wa eneo hilo wakiwa hawana mahali pa kuishi.
Share:

Maagizo Aliyoyatoa Rais Magufuli Baada ya Kufanya Ziara ya Kushtukiza Katika Gereza la Ukonga

Maagizo Aliyoyatoa Rais Magufuli Baada ya Kufanya Ziara ya Kushtukiza Katika Gereza la Ukonga

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Jumanne  tarehe 29 Novemba , 2016  amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar Es Salaam  na kupiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.

Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi nchini na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi ya hapa nchini
 
Hali kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika. 
 
''Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu , amesema Rais magufuli'' 
 
Aidha Rais Magufuli ametoa shilingi Bilioni Kumi kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam. 
 
Hatua hiyo inafuatia kilio cha askari Magereza kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uaraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi nchini na hata kuzorotesha utendaji kazi wa askari wa Jeshi hilo. 
 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia ameagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika katika uzalishaji mali badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi ya wafungwa wamekuwa  wakitutumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.
 
 Rais Magufuli amewahakikishia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine nchini. 
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na  Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam  Novemba 29, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi  na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikaribishwa na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja ili aongee  na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016
 Mmoja wa askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza akitoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli  alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akichukua maelezo kutoka kwa  maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Novemba 30

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Novemba 30


Share:

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages