Makamu wa Rais Asema Serikali Itaendelea Kushirikiana na Wadau Mbalimbali Kuhakikisha Rasilimali ya Gesi Inakuza Uchumi wa Taifa

Makamu wa Rais Asema Serikali Itaendelea Kushirikiana na Wadau Mbalimbali Kuhakikisha Rasilimali ya Gesi Inakuza Uchumi wa Taifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha rasilimali ya gesi na mafuta inakuwa ni chachu ya kukuza uchumi wa taifa na wa wananchi kwa ujumla.
 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo jana 22-Nov-2016 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa mwaka wa kujadili masuala ya gesi na mafuta barani Afrika ulioandaliwa na Kampuni ya Getenergy ya Uingereza.
 
Katika hotuba yake, Makamu wa Rais aliwahakikishia washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi na itakuwa bega kwa bega na wadau wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha uwekezaji utakaofanyika unakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.
 
Alisisitiza kuwa kwa sasa Serikali ya Tanzania inaendelea na mkakati  kabambe wa kusomesha wataalamu wa fani ya mafuta na gesi ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha taifa linajitosheleza kwa wataalamu hao ambao watakuwa na uwezo na ujuzi wa kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa katika sekta za gesi na mafuta.
 
Makamu wa Rais alisema Tanzania imegundua kiasi kikubwa na gesi na ana imani kubwa kuwa mafuta nayo yanapatikana hivyo ni muhimu kwa mataifa ya Afrika  kujipanga kuwa na wataalamu wake wazalendo wa kutosha watakaoshikiri katika uchumi wa gesi na mafuta kwa kuajiriwa kwenye makampuni yanajihusisha na utafiti na
uchimbaji wa gesi na mafuta.
 
Asema anaimani kubwa kuwa rasilimali ya gesi na mafuta zitakazogundulika na kuchimbwa barani Afrika zitasaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa mataifa hayo, uchumi ambao utasaidia  kuimarisha utoaji wa huduma bora za kijamii kwa wananchi katika nchi husika.
 
Mkutano huo wa siku Mbili wa Kimataifa umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya gesi na mafuta kutoka ndani na nje ya nchi ambao wanajadili kwa kina na kubadilishana uzoefu kuhusu njia bora za uwekezaji katika sekta hiyo barani Afrika.
 
Kwa upande wake,Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alisisitiza kwa Serikali itaendelea kusomesha wataalamu wake ndani na nje ya nchi ili kujitosheleza kwa wataalamu wa sekta hiyo.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages