Trump na Obama watofautiana kuhusu Fidel Castro
Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, amemtaja Fidel Castro kama nduli na mdhalimu aliyewatesa watu wake kwa miongo kadhaa na kuwa ameacha kumbukumbu yenye machungu mengi kwa watu wa Cuba.
Lakini Rais Obama alisema kuwa anawapa mkono wa urafiki watu wa Cuba, akisema serikali yake imefanya kila juhudi kuangamiza uhasama kati ya mataifa yao mawili.
Katika kampeni yake Bwana Trump alitisha kusitisha uhusiano bora unaoendelea kuimarika kati ya Cuba na Marekani.
Uhusiano wa kibalozi kati ya Marekani na Cuba ulirejeshwa Julai Mwaka uliopita kufuatia juhudi za rais Barack Obama.
No comments:
Post a Comment