Godbless Lema Anyimwa Dhamana Kwa Mara Nyingine Tena
Mbunge
wa Arusha Mjini Godbless Lema amekwaa kisiki kwa mara nyingine katika
harakati za kuomba dhamana baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha
kutupilia mbali ombi la marejeo ya kesi yake na kushauri kuwa Mawakili
wake wakate rufaa ya kupinga zuio la dhamana
Mawakili
wa Lema leo walikuwa wakirusha karata hiyo kwa mara ya tatu baada ya
mara mbili za awali mteja wao kushindwa kupata dhamana.
Lema
amesota rumande tangu alipokamatwa Novemba 3, 2016 akiwa mkoani Dodoma
na kusafirishwa hadi Arusha ambapo anashtakiwa kwa kosa la uchochezi
dhidi ya Rais Dkt Magufuli.
No comments:
Post a Comment