Hatima ya dhamana ya Godbless Lema kujulikana leo
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, leo, anatarajia kujua hatima ya dhamana ya kesi ya uchochezi inayomkabili.
Lema anashikiliwa katika mahabusu ya Magereza ya Kisongo mjini Arusha.
Wakili wake, Peter Kibatala amesema walikata rufaa chini ya hati ya dharura kuomba Mahakama isikilize kesi hiyo mapema.
Amesema
waliamua kufuata maelekezo ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda
ya Arusha, Sekela Mosha ya kuwataka kukata rufaa.
Katibu
wa mbunge huyo, Innocent Kisanyage amesema rufaa hiyo itasikilizwa leo
saa tatu asubuhi baada ya kukamilisha mambo yanayotakiwa.
Lema
alirudishwa mahabusu kutokana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kukataa
kupokea ombi lake la kufanya marejeo ya uamuzi wa kunyimwa dhamana.
Kaimu
Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mosha alisema uamuzi uliofanywa na
Mahakama ya Hakimu Mkazi umeegemea kifungu cha Sheria cha Makosa ya
Jinai CPA 148, hivyo kilimtaka mshtakiwa kukata rufaa siyo kuomba
Mahakama hiyo kufanye rejea,
Rufaa hiyo itasikilizwa na Jaji Fatuma Massengi, huku Lema akitimiza siku ya 26 tangu apelekwe Gereza la Kisongo.
No comments:
Post a Comment