Rais Magufuli amualika Rais wa Zambia kwa ziara ya siku 3
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.
Augustine Mahiga, amesema Rais Edgar Lungu wa Zambia anatarajiwa kufanya
ziara rasmi ya siku tatu nchini kuanzia Novemba 27 kwa mwaliko wa Rais
Dkt. John Pombe Magufuli.
Dkt. Mahiga amesema wakati wa ziara hiyo, Rais Lungu atasaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Zambia na Tanzania.
Miongoni
mwa mikataba hiyo ni pamoja na ushirikiano wa masuala ya anga, ulinzi
na usalama, ushirikiano katika masuala ya uhamiaji, na kuweka utaratibu
wa kubadilishana wafungwa.
Akiwa nchini Rais Lungu pia atatembelea Bandari ya Dar es Salaam, reli ya Tazara, na bomba la mafuta la Tazama.
Kwa
upande wake Mkurugenzi idara ya Afrika Balozi Samweli Shelukindo
amesema utekelezaji wa mikataba hiyo utaleta maendeleo baina ya nchi
hizi mbili.
No comments:
Post a Comment