Wafuasi wa CUF Watwangana Ngumi Mahakamani
Wafuasi
wa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa Chama
hicho, Maalim Seif Sharif Hamad jana waligeuka sinema ya bure baada ya
kutwangana makonde hadharani katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya
Dar es Salaam.
Ugomvi
huo ulioibua mapambano ya ngumi ulitokea jana baada ya wafuasi wa
Maalim Seif waliokuwa mahakamani hapo kumzuia Profesa Lipumba kuingia
kusikiliza kesi inayomkabili iliyofunguliwa na Baraza la Wadhamini wa
Chama hicho.
Profesa
Lipumba alifika mahakamani hapo saa mbili asubuhi, ikiwa ni mara yake
ya kwanza tangu kesi hiyo dhidi yake kufunguliwa ikidai kuwa yeye si
mwanachama halali wa CUF.
Baada
ya kesi za Jaji Sakiet Kihio kuitwa na mtoa matangazo wa Mahakama kwa
kuelekeza kuwa kesi za Jaji huyo zinasikilizwa chemba watu wote
waliinuka na kuelekea katika chumba hicho wakiwamo mawakili wa pande
zote.
Walipofika
kwenye mlango wa chumba cha Mahakama, wafuasi wa Maalim Seif walisimama
mlangoni kumzuia Profesa Lipumba kwa madai kuwa wanaotakiwa ni mawakili
tu na si watu wengine, ndipo wafuasi wa Mwenyekiti huyo walipoingilia
kati na kuwashushia kipigo watu hao.
Hatua
hiyo ilishuhudia mabadilishno ya makonde na kusababisha watu wawili
upande wa Maalim Seif kuumia, na kusababisha Jaji Kihio kutoa amri kuwa
waingie mawakili na walalamikiwa ndipo Lipumba naye akaingia.
Kesi
iliendelea kusikilizwa, huku askari wakiimarisha ulinzi wa chumba
hicho, kwa sababu wakati wafuasi hao wanapigana wao hawakuwapo. Jaji
Kihio aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 6 zitakaposikilizwa sababu za
Bodi hiyo kumtaka ajitoe kusikiliza kesi hiyo.
Baada
ya kesi hiyo kuahirishwa, Profesa Lipumba alitolewa na wafuasi wake
akiwa chini ya ulinzi mkali kwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakayemgusa
na alipofika nje, alipokewa na wafuasi wengine wakiwa na mabango yenye
ujumbe dhidi ya Maalim Seif.
Bango
moja liliandikwa: ‘Maalim Seif kama ulikaa na CCM umeshindwaje kukaa na
Mwenyekiti wako Lipumba mkayamaliza’, lingine: ‘Maalim Seif tulijua CCM
ndiyo kiboko yako, kumbe Lipumba ndiye mwamba wako’, huku wakiendelea
kuimba wimbo wa chama hicho.
Lipumba
alipoingia kwenye gari alishusha kioo na kusalimu wafuasi wake kwa
kuwapungia mikono, huku wengine wakisukuma gari lake kabla ya kuondoka
eneo la Mahakama.
Hata
hivyo, Profesa Lipumba hakutaka kuzungumza chochote, akitumia muda wake
mwingi kutabasamu na kupunga mkono. Wakati hayo yote yakifanyika, nje
ya Mahakama askari walikuwa tayari wametenga makundi hayo mawili, lakini
bila kufanya hivyo, watu hao wangeendelea kupigana.
Wakili
wa Bodi hiyo, Juma Nassoro akiwa nje ya Mahakama, alimkariri Jaji
akisema Desemba 6 kesi hiyo ataisikilizia kwenye Mahakama ya Wazi, kwa
sababu alikuwa hajui kama watu ni wengi, kwa hiyo hataifanyia tena
chemba.
Pia
alisema Profesa Lipumba, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis
Mutungi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na wafuasi 11
wamewasilisha pingamizi mahakamani hapo, kuwa wateja wake walifungua
kesi hiyo bila idhini ya Mahakama na pia Maalim Seif alibariki
kufunguliwa kwa kesi hiyo bila idhini ya Bodi.
Baadaye
mawakili wa CUF, Nassor na Hashimu Mziray waliwasilisha ombi la kumtaka
Jaji Kihiyo ajitoe kusikiliza shauri hilo kwenye Mahakama hiyo, na
sababu za kumkataa zitaelezwa Desemba 6 saa saba mchana wakati kesi hiyo
itakapokuja kusikilizwa.
Walalamikaji
hao wanaomba Mahakama itengue barua ya Msajili ya kumtambua Profesa
Lipumba kuwa mwanachama hai wa CUF. Wakili Mziray alisema walifungua
kesi hiyo kwa hati ya dharura kutokana na mambo yalivyo sasa ndani ya
chama hicho, kwa sababu hawajui hata ofisi zingine zinaendeshwaje.
Alisema
katika maombi hayo, wanaiomba Mahakama mambo matatu, ambayo ndiyo
yanasababisha kufukuta kwa mgogoro, kwa hiyo wanaomba yatenguliwe ili
shughuli za kisiasa ziendelee.
Alisema
mambo hayo ni pamoja na Mahakama kutengua barua ya Msajili ya Septemba
23 ambayo ilitengua uamuzi wa CUF wa kumfukuza uanachama Profesa Lipumba
na kumhalalisha kuwa mwanachama hai wa chama kama Mwenyekiti.
No comments:
Post a Comment