Baba Wa Kambo Atiwa Mbaroni kwa Kumnajisi Hadi Kufa Mtoto wa Miaka Mitatu

Baba Wa Kambo Atiwa Mbaroni kwa Kumnajisi Hadi Kufa Mtoto wa Miaka Mitatu


Mtoto  mdogo mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Kijiji cha Nyamihaga Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma amekufa baada ya kunajisiwa na baba yake wa kambo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kwamba wamemtia mbaroni mtuhumiwa Hamimu Saidi (27) mkazi wa kijiji hicho cha Nyamihaga.

Akitoa maelekezo kuhusu mkasa huo, Kamanda Mtui alisema mtuhumiwa alitekeleza dhamira yake hiyo wakati mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa mke wa mtuhumiwa alipokwenda kisimani kuchota maji.

Alisema baada ya mwanamke huyo kurejea nyumbani kutoka kisimani alimshuhudia mtoto wake akilalamika sana wakati akitaka kujisaidia haja ndogo na ndipo alipomchunguza akagundua kwamba mtoto huyo alikuwa ameingiliwa na kujeruhiwa kwenye sehemu zake za siri.

Kamanda Mtui alisema baada ya kugundua hilo, mama huyo wa mtoto alimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitali ya Mkoa ya Maweni kwa matibabu, ambako iligunduliwa kuwa mtoto huyo alikuwa amenajisiwa na alikuwa amebanwa shingo wakati akifanyiwa kitendo hicho hivyo alikosa pumzi wakati akifanyiwa unyama huo.

Kamanda huyo alisema hata hivyo mtoto huyo alifariki katika Hospitali ya Mkoa ya Maweni alipokuwa akitibiwa na kwamba baada ya uchunguzi wa kidaktari na uchunguzi wa Polisi, mwili wa mtoto huyo ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

“Kwa sasa mtuhumiwa Hamimu Saidi anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Kigoma wakati upelelezi ukiendelea ili taratibu za kumfikisha mahakamani zifanyike na kwamba anatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi huo utakapokamilika,” alieleza Kamanda Mtui.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages