Mwenyekiti aomba kupigwa risasi mbele ya Makonda
Katika hali ya kushangaza, jana Mwenyekiti wa soko la Mbande Mbagala katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mokiwa Hassani aliomba kupigwa risasi mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kutuhumiwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha katika upangishaji wa vizimba sokoni hapo.
Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kufika sokoni hapo kwaajili ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika manispaa ya Temeke.
Kufuatia tuhuma hizo ikamlazimu mkuu wa mkoa kumsimamisha mwenyekiti wa soko hilo Hassani ili kujibu tuhuma hizo ndipo alipotoa kauli hiyo na kufafanua kuwa bei hiyo ya shilingi laki nne kwa kizimba ni makubaliano kati yao na wananchi hao, pia fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kuendesha soko hilo, ambalo bado halijakabidhiwa kwa Halmashauri.
Kufuatia utetezi huo ikamlazimu Mkuu wa Mkoa kutumia busara ambapo aliuagiza mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kusimamia uundwaji wa uongozi wa soko hilo haraka mpaka kufikia mwezi Desemba kero zinazolikabili soko hilo ziwe zimetatuliwa.
No comments:
Post a Comment