Kampeni ya kumng’oa Trump yashika kasi
Ndoto
za Donald Trump aliyechaguliwa hivi karibuni kuwa Rais wa 45 wa
Marekani huenda zikayeyuka baada ya wajumbe sita wa Democratic
watakaopiga kura za majimbo kuanzisha kampeni maalumu ya kuwashawishi
wajumbe wengine kutomwidhinisha Rais huyo mteule.
Wajumbe
hao ambao majina yao yalitangazwa jana wanaamini kuwa iwapo
watafanikiwa kuwashawishi wenzao wengine 37 kutoka Chama cha Republican
basi watakuwa wamefanikiwa kumzuia bilionea huyo kuingia ikulu.
Desemba
19 wajumbe 538 kutoka majimboni watakutana kupiga kura ya kisheria
kumthibitisha Rais mteule anayetarajiwa kuapishwa Januari 20. Kura hizo
zitahesabiwa mbele ya Bunge la Congress Januari 6.
Hatua
ya wajumbe hao wa Democratic kuanzisha kampeni hiyo imekuja siku chache
baada ya makundi ya kiharakati kuanza kukusanya saini nchi nzima ili
kuwashinikiza wajumbe hao kutompitisha rais huyo ambaye tayari ameanza
kutangaza vipaumbe vyake.
Mmoja
wa wajumbe hao aliyetambulika kwa jina la Michael Baca anayewakilisha
Colorado amekuwa akizunguka huku na kule kuwashawishi wajumbe wenzake
kuepuka kumuunga mkono Trump wakati wa upigaji wa kura.
Mjumbe
mwingine ambaye hakupenda jina lake kutajwa alisema kutokana na mvutano
unaoendelea kujitokeza sasa kunaweza kuzusha hoja zitakazolazimisha
kuangaliwa upya kwa mfumo unaotumika sasa kupitia kura za majimbo
kumchagua rais.
Ingawa
bado haijajulikana ni wajumbe wangapi wanaendelea kuwa waaminifu kwa
kambi ya Trump lakini mchambuzi wa masuala ya siasa, Profesa George
Edwards III amesema kama kutatokea wajumbe nane au 10 wakaamua
kutomuunga mkono rais huyo mtarajiwa basi kunaweza kubadilisha ndoto za
kiongozi huyo kuingia ikulu Januari 20 mwakani.
Tayari
wafuasi hao wameitisha kampeni ya kuomba Wamarekani kuwaunga mkono
mtandaoni kupitia tovuti ya www.change.org wa kuwashawishi wachaguaji
hao kumchagua Clinton badala ya kumthibitisha Trump kwa kuwa hafai kuwa
rais wa taifa hilo.
Ujumbe huo unaeleza kuwa iwapo watachagua kama ambavyo majimbo yamepiga kura katika uchaguzi huu, Trump atashinda.
“Hata
hivyo, wanaweza kumpigia Hillary Clinton wakiamua,” inasomeka sehemu ya
kampeni hiyo yenye kichwa cha habari; “Kura ya uamuzi: Mfanye Hillary
Clinton kuwa rais Desemba 19”.
“Hata
katika majimbo ambayo wajumbe hawatakiwi kufanya hivyo, wakiamua kura
zao zitahesabika, wanaweza wakafanya uamuzi kidogo ambao tutaamini
wafuasi wa Clinton watavutiwa nao.”
Mtandao
huo unaeleza kuwa Clinton alishinda kura ya wengi hivyo anafaa kuwa
rais kwa kuwa Trump alishinda majimbo yenye kura nyingi za majimbo basi
mwenendo ukaonyesha bayana kuwa atashinda kura za uamuzi.
Katika
uchaguzi uliofanyika Novemba 8 mwaka huu, Wamarekani waliwachagua
wagombea wa urais kwa kura ya wengi na kuchagua wapigakura
watakaomchagua rais mteule mwezi mmoja ujao.
Clinton
aliongoza kura za wengi kwa zaidi ya kura 200,000 lakini Trump aliibuka
mshindi kutokana na kushinda majimbo yenye kura nyingi za majimbo.
Ili Rais ashinde kinyang’anyiro hicho, anatakiwa kushinda kura 270 kati ya kura 538 zilizopo kutoka majimboni.
Kwa
kutumia mfumo wa mshindi wa jimbo anashinda pia kura za uamuzi. Hadi
sasa Trump ana kura 306 wakati mpinzani wake, Clinton akiondoka na kura
232. Ni mara chache kwa Marekani mshindi wa urais kuzidiwa katika kura
za wengi.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Fordham, Christina Greer alisema kati ya wajumbe 538
watakaopiga kura mwaka huu, 100 ni maseneta ambao ni wawili kila jimbo,
wajumbe watatu kutoka makao makuu ya nchi, Washington D.C, na wabunge
435.
“Majimbo
yote kasoro mawili ya Maine na Nebraska mgombea mwenye kura nyingi
kwenye jimbo basi ndiye mshindi pia wa kura za wajumbe.
“Hii
ina maana matokeo yakitoka tu mwenye kura nyingi huwa ni mshindi licha
ya kura kusubiri kura za uamuzi Desemba 19,” Dk Dreer.
Hata
hivyo, matumaini ya wafuasi hao wa Clinton huenda yasizae matunda kwa
kuwa sheria za majimbo mengi likiwamo la Minnesota Marekani zinakataza
uwepo wa “wajumbe wasiowaaminifu” na baadhi yanatoza faini kati ya Dola
500 (Sh1 milioni) za Marekani hadi 1,000 (zaidi ya Sh2 milioni).
Faini
hiyo ni matokeo ya uamuzi wa Mahakama juu ya nchi hiyo iliamua mwaka
1952 wapigakura hao wawe wanakula viapo mapema wakati wa mkutano mkuu wa
chama juu ya nani watamchagua, mtandao wa Factcheck.org unaochapisha
habari za siasa, umeeleza.
No comments:
Post a Comment