Trump aahidi Marekani kujitoa kwenye Saa moja iliyopita
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema kuwa siku yake ya kwanza madarakani atatoa tamko la kujiondoa katika mpango wa biashara ya ubia ya nchi za Pasifiki.
Mkataba wa kibiashara wa mataifa ya Pasifiki uliafikiwa mwaka 2015 na Marekani, Japan, Malaysia, Australia, New Zealand, Canada na Mexico, miongoni mwa nchi nyingine lakini haujaanza kutekelezwa na nchi husika.
Katika ujumbe wa video wa mipango yake kwa ajili ya siku yake ya kwanza ,alisema ingekuwa badala yake kujadili mikataba ya biashara ya pande mbili ili kuleta ajira na viwanda kurudi Marekani.
Trump amesema atajikita kwenye kukatisha vizuizi vya makaa ya mawe na kuendeleza mpango wa kulinda miundombinu muhimu.
Ushirikiano wa nchi za Pasifiki ulisainiwa mwezi Februari baada ya miaka saba ya mazungumzo na ilikuwa msingi wa sera ya biashara ya Rais Obama.
Mkataba huo ulitiwa saini na mataifa 12 ambayo kwa pamoja hudhibiti asilimia 40 ya uchumi wa dunia.
Bw Trump pia ameahidi kupunguza masharti ya kiserikali "yanayoua" uzalishaji wa makaa ya mawe na pia kuzuia watu kutumia vibaya sheria ya visa.
Hata hivyo, hakugusia mpango wake wa kubatilisha mpango wa huduma ya bima ya afya wa Obamacare pamoja na mpango wa kujenga ukuta mpaka wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji kutoka taifa hilo jirani wasiingie Marekani.
Mambo hayo mawili alikuwa amesema mambo hayo mawili atayafanya haraka iwezekanavyo baada ya kuingia madarakani.
Mambo mengine Trump ameahidi kuyafanya siku ya kwanza:
- Kuondoa vikwazo vya uzalishaji wa kawi Marekani
- Kupunguza sheria zinazosimamia biashara Marekani
- Kuamrisha mpango wa kukabili mashambulio ya mtandaoni
- Kuchunguza matumizi mabaya ya sheria ya visa ambayo huwadhuru wafanyakazi wa Marekani
- Kuweka marufuku ya miaka mitano kuzuia watu wanaotoka serikalini kuwa watetezi wa masuala mbalimbali ya kisiasa
No comments:
Post a Comment