Shilingi bilioni 3 zatafunwa kununulia mafuta katika 'magari hewa' .
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Luteni Kanali Mstaafu Dkt. Haroun Kondo (Kushoto)
**
Bodi
ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania imeuagiza uongozi wa
shirika hilo kuwatambua na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria,
wafanyakazi wake waliolisababishia shirika hilo hasara kupitia mikataba
ya kilaghai pamoja na utendaji mbovu
Mwenyekiti
wa Bodi hiyo Luteni Kanali Mstaafu Dkt. Haroun Kondo, ametoa agizo hilo
jana wakati akitoa taarifa kuhusu utiaji saini ya makubaliano ya
kiutendaji kati ya bodi ya wakurugenzi na uongozi juu wa shirika hilo
kuhusu jinsi wanavyopaswa kuliendesha shirika hilo kwa faida.
Kwa
mujibu wa Dkt. Kondo, ubadhirifu ndani ya shirika hilo umevuka mipaka
na kamwe hauwezi kuvumilika ambapo alitaja baadhi ya mianya ya wizi kuwa
ni katika uendeshaji na usimamizi wa rasilimali za shirika.
Alitolea
mfano jinsi shilingi bilioni tatu zilivyotafunwa na wajanja wachache
kwa kisingizio cha malipo ya mafuta kwa magari ambayo taarifa zake
zinaonesha kuwa hayatembei kutokana na kuwa katika matengenezo kwa muda
mrefu.
No comments:
Post a Comment