Kanye West 'alazwa hospitalini Los Angeles'
Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Kanye West amelazwa hospitalini mjini Los Angeles, vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti.
Msemaji wa polisi ameambia BBC kwamba walipokea simu ya kutokea kwa mtafaruku Jumatatu adhuhuri, lakini hawakutaja jina la mwanamuziki huyo.
Baadaye, mtafaruku huo ulidaiwa kuwa tukio la kimatibabu, na maafisa wa kutoa huduma ya dharura walifika eneo hilo.
Msemaji wa maafisa wa huduma za dharura wa LA amesema mwanamume ambaye jina lake halikutajwa alipelekwa hospitalini "kufanyiwa uchunguzi zaidi".
"Mwendo wa saa 13:20 majira ya kanda ya pasifiki, idara ya huduma za dharura ya Los Angeles ilipokea ombi la dharura la huduma ya matibabu ambalo halikuelezwa kwa kina," amsemaji huyo alisema.
"Mwanamume mzima, ambaye hali yake ya afya ni thabiti, alipelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi zaidi."
NBC news wanasema hatua ya kumlaza West imechukuliwa kwa ajili ya afya yake na usalama wake.
Tovuti ya udaku ya TMZ imesema West amepelekwa hospitali kufanyiwa "uchunguzi wa kiakili" na kwamba amekuwa akitafuta matibabu "kwa sababu ya kukosa usingizi sana".
Los Angeles Times imeripoti kwamba kulipigwa simu ya 911 kutoka nyumba ya Kanye West.
West nawawakilishi wake hawajazungumzia tukio hilo.
Mkewe, Kim Kardashian, alitarajiwa kuhudhuria hafla fulani New York Jumatatu, mara yake ya kwanza kutokea hadharani tangu avamiwe na wezi Paris mwezi Oktoba, lakini hakufika.
West alikuwa amefuta tamasha zote zilizokuwa zimesalia kwenye ziara yake ya sasa ya kimuziki.
Alikuwa ameondoka tamasha ya Sacramento ikiwa katikati wikendi.
Alikuwa ameimba nyimbo tatu pekee Jumamosi usiku kabla ya kuanza kuwafokea watu na kushambulia Facebook, Jay Z na Hillary Clinton.
Alimkosoa mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg kwa kukosa kumlipa $53m (£42.5m) alipe madeni.
Alisema pia kwamba alikereka sana na hatua ya Jay Z na familia yake kutomtembelea baada ya mkewe kuporwa Paris mwezi Oktoba.
No comments:
Post a Comment