Jiji la Mbeya ni la pili kwa wingi wa madhehebu barani Afrika likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.
Jiji la Mbeya ni la pili kwa wingi wa madhehebu barani Afrika likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika, jiji hilo lina
makanisa 450 na Mtaa wa Sae pekee una madhehebu tisa huku Mtaa wa
Simike ukitajwa kuongoza kwa vituo vya maombezi.
Meya
wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi ambaye ni kiongozi wa
Kanisa la International Evangerism Assemblies of God, amesema migogoro
ndani ya madhehebu, uroho wa madaraka na utapeli ni miongoni mwa sababu
ya watu kuamua kuanzisha madhehebu kila kukicha.
Meya
huyo ambaye pia ni msimamizi wa kanisa hilo katika mikoa ya Ruvuma,
Iringa, Njombe na Rukwa, amesema hakuna ubaya wa kuwa na madhebu mengi
kama yanaanzishwa kwa kufuata utaratibu, sheria na misingi ya Mungu.
Amesema
madhehebu mengi ya kilokole jijini humo yaliibuka baada waamini kuamua
kujitenga madhehebu yao ya awali kutokana na migogoro.
“Kuna
madhehebu yanamiliki vyuo vya wachungaji wanaosomea kwa mujibu wa
maadili ya Mungu, kama Lutherani, Wakatoliki, Moravian, Wasabato na la
kwangu, lakini tatizo wapo wachungaji wa kujipachika ambao mara nyingi
wanatiliwa shaka kwa vitendo vyao,” amesema meya huyo.
No comments:
Post a Comment