RC Makonda Aamuru Mwenyekiti wa Mtuu Akamtwe na Kuwekwa Rumande Hadi Upelelezi Utapokamilika

RC Makonda Aamuru Mwenyekiti wa Mtuu Akamtwe na Kuwekwa Rumande Hadi Upelelezi Utapokamilika

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda jana  aliliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Gongolamboto, Bakari Shingo baada ya kutuhumiwa kukusanya mapato kwa kutumia risiti anazozichapisha mwenyewe kinyume na Halmashauri inavyoagiza pamoja na kutoitisha mikutano ya hadhara kwa muda mrefu na kushirikina na wahalifu.
 
Hatua hiyo ilikuja baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kukaa muda mrefu bila kusoma mapato ya mtaa huo pamoja na kughushi stakabadhii za mapato.

Lawama hizo zilimpelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye alikuwa  kwenye ziara yake katika wilaya ya Ilala Pugu Kajiungeni, kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni kumsweka rumande Mweyekiti huyo mpaka upelelezi utakapo kamilika.

Akitoa ushahidi kuhusu sakata hilo Mkazi wa Gongo la Mboto na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Pili Seif alieleza kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya mwenyekiti huyo kwa muda mrefu na taarifa zimefikishwa kwenye mamlaka husika ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, Mkurugenzi Msongela Nitu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages