Makomba Asubiri Kibali cha Rais Kuwafuta Kazi wa Watumishi wa Umma Dar...

Makomba Asubiri Kibali cha Rais Kuwafuta Kazi wa Watumishi wa Umma Dar...

Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema itawastaafisha kwa manufaa ya umma watumishi wa mkoa huo walioshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Hayo yalisemwa jana jijini humo na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Temeke akiwa katika ziara ya siku mbili wilayani humo. Alisema watumishi wengi wamekuwa mizigo na wanasubiri kuchukua mishahara bila kuifanyia kazi hivyo ni bora kuwasimamisha kwa manufaa ya umma.

“Nafikiri kuna haja ya kuwapunguza watumishi serikalini hakuna wanachofanya zaidi ya majungu na umbea, asilimia 20 ndio wanaofanya kazi, tayari nimeongea na Rais na kuna taratibu nakamilisha na tutachukua hatua,” alisema Makonda.

Aidha Makonda alisema watumishi wengi wa umma wanaishia kula fedha za miradi na matokeo yake wanatengeneza miradi mibovu ambayo imekuwa ikichukuwa muda mfupi kuharibika.

Makonda aliwashangaa watumishi wanaoshindwa kufanya kazi na kudai hawana bajeti wakati wana uwezo wa kuzungumza na wadau na kupata fedha nyingi na kuendesha miradi.

“Tumechoka kusikia kelele za kukosa bajeti, yapo mambo hayahitaji bajeti lakini hamfanyi tangu kuteuliwa kwangu nimeweza kufanya miradi ya zaidi ya Sh bilioni 30 ambayo sio ya bajeti, lakini nyinyi mnapiga kelele za bajeti, tukiona hamuwezi kubadilika tutawastafisha tunataka watu wanaofikiria nje ya boksi,” alisema Makonda.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages