Kauli Ya mwisho ya Samwel Sitta Baada ya Daktari kumueleza kuwa Asingeweza Kupona

Kauli Ya mwisho ya Samwel Sitta Baada ya Daktari kumueleza kuwa Asingeweza Kupona


Kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanza nia (2005-2010), Samuel Sitta, mwanae wa kiume ameweka wazi maneno matatu ya mwisho aliyoyatamka, yenye maana nzito katika maisha.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye ni mtoto wa kiume wa marehemu, alisema kuwa baba yake alitoa maneno matatu ya kuukubali ukweli wa maisha baada ya Daktari kumueleza kuwa asingeweza kupona.

“That’s life (hayo ndiyo maisha),” Benjamin alikariri maneno ya baba yake. Alisema hayo yalikuwa maneno yake ya mwisho baada ya kuelezwa ukweli na daktari wa hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu.

Maneo ya Sitta ni funzo kubwa kwa watu wote kuwa maisha huanza na huisha, hiyo ndiyo maana ya maisha na hakuna aishie milele hivyo tuishi kwa kuzingatia maana hiyo ya maisha na kuikubali.

Sitta ambaye anakumbukwa kwa kauli mbiu yake na matendo ya kusimamia ‘kasi na viwango’, alifariki kutokana na ugonjwa wa tezi dume uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Alitangaza kustaafu siasa muda mfupi baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ambapo yeye alikuwa mmoja kati ya waliokuwa msitari wa mbele kumnadi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo.

Benjamini alieleza kuwa marehemu atazikwa Urambo Mkoani Tabora na kwamba ratiba ya mazishi itatolewa na Ofisi ya Bunge ambayo ndiyo inayoratibu mazishi

“Tumempoteza baba na kiongozi ambaye tulikuwa tunamtegemea kwa ushauri na masuala mbalimbali, tutafuata yale aliyokuwa akituelekeza,”alisema Benjamini.

Hakika Taifa limempoteza mtu muhimu, pengo lake halitazibika kamwe. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages