Mji wa Aleppo wakumbwa na mashambulizi makali
Maafisa wa Afya katika mji wa Alleppo nchini Syria wamelazimika kusitisha huduma za hospitali katika eneo la mashariki linaloshikiliwa na waasi kufuatia siku kadhaa za mashambulizi makali ya mabomu.
Mkurugenzi wa huduma za matibabu mashariki mwa Aleppo Abdul Baset Ibrahim, amelaumu mashambulizi ya saa arubaini na nane ya ndege za kivita za Urusi na Syria dhidi ya maeneo yanayokaribiana na mahospitali.
Hapo jana kulikuwa na ripoti kuwa hospitali ya watoto imelengwa huku kukiwa na hofu kwamba shabulio hilo lilikuwa ya gesi ya chlorine.
Mshauri wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Jan Egeland, amesema wakaaazi wa Aleppo wanakabiliwa na hali ngumu.
Mapema wiki hii Urusi imekanusha kufanya oparesheni katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment