Rais Magufuli Awataka Watanzania Kutumia Fursa Zilizopo

Rais Magufuli Awataka Watanzania Kutumia Fursa Zilizopo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka watanzania kutumia fursa zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa ajili ya kuliletea maendeleo ya taifa.

Aliyasema hayo jana Jijini Dar es Saalam wakati wa mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya habari nchini katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Utawala wake, ambapo alisema kuwa ipo haja ya kuzungumza na kuelimisha watanzania juu ya fursa zilizopo katika taasisi hizo.

“Katika Jumuiya hizo zipo fursa nyingi kwa ajili ya maendeleo ingawa inahitajika elimu ya kutosha kwa watanzania kuona fursa zilizopo ikiwemo ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchi za nje” alisema Rais Magufuli.

Mbali na hayo, akizungumza kuhusu suala la kupambana na Rushwa nchini Rais Magufuli alitoa wito kwa vyombo vinavyohusika na kupambana na rushwa kufichua watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Rais Magufuli alisema kuwa vita ya Rushwa ni ya kila mwananchi, ambapo alitoa wito kwa watanzania wote kwa ujumla kujiepisha na masuala ya rushwa kwani rushwa ni kansa ya maendeleo nchini.

“Taifa litakwama tukiacha suala la rushwa liendelee, tumeumia kweli kweli katika hili hivyo nitoe wito kwa watanzania wote kwa ujumla kujiepusha na masuala haya kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwani kesi ya rushwa ni yetu sote” alifafanua Rais Magufuli.
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages