Ushindi wa Trump Waacha Kilio Bungeni Dodoma

Ushindi wa Trump Waacha Kilio Bungeni Dodoma


Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema wabunge wanawake wamesikitishwa na kushindwa kwa mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Democrat, Hillary Clinton.

Dk. Tulia alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana, baada ya kutambulisha wageni mbalimbali.

Alisema walitarajia mambo yangekuwa mazuri upande wao  akiwa mama (wanawake), lakini haikuwezekana.

“Safari hii haikuwezekana, asikate tamaa maana baada ya miaka minne mambo yanaweza kuwa mazuri zaidi kuliko ilivyokuwa sasa. Nampa pole mama Clinton kwa kuwa safari hii haikuwezakana,”alisema Dk Tulia huku akishangiliwa na wabunge wanawake na kuongeza:

“Nasikia kuna watu hapa wanasema tungempeleka mheshimiwa fulani… katika maeneo yale mama Clinton angeshinda,” alisema.

Kutokana na kile kilichoonekana kupigwa butwaa na uchaguzi huo, kabla ya kuuliza swali la nyongeza jana asubuhi, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema), alisema ana masikitiko makubwa kwa sababu Hillary Clinton ameshindwa uchaguzi.

“Kwa niaba ya wanawake wenzangu, nampa pole mama Clinton kwa kushindwa uchaguzi, tumeumia sana na tumerudi nyuma,” alisema.

Kauli hiyo ilimfanya Dk. Tulia kumtaka aeleze amepata wapi taarifa wakati bado wabunge wanawake wana faraja  Hillary angeweza kushinda.

Hata hivyo, akijibu swali la Suzan, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangala,  alimpa pole Hillary kwa kushindwa kwenye uchaguzi huo.
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages