Ziara Ya Makamu Wa Rais Mhe.samia Yawa Na Mafanikio Ukerewe

Ziara Ya Makamu Wa Rais Mhe.samia Yawa Na Mafanikio Ukerewe


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji kwenye mji Nansio katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza mradi ambao utahudumia wananchi elfu 61.

Makamu wa Rais ambaye jana  alisafiri kwa takribani masaa Matatu na meli ya MV Nyehunge II katika Ziwa Victoria kwenda kisiwa hicho kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo,aliwahimiza wananchi hao wautunze mradi huo ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo na uhaba wa maji safi na salama katika kisiwa hicho.
 
Mradi huo ambao unaojumuisha kazi za uboreshaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira unatekelezwa chini ya umefadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na serikali ya Tanzania katika miji ya Sengerema,Geita na Nansio – Ukerewe kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 30.4 ambapo serikali ya Tanzania imechangia mradi huo Dola za Kimarekani milioni nne.
 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliwaahidi wananchi kuwa serikali ya awamu ya Tano inamikakati mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini  ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji. 
 
Akihutubia mamia ya wananchi  wa kisiwa cha ukerewe kwenye kijiji cha Kagunguli mkoani Mwanza mara baada ya kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili  ukiwemo mradi wa maji na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Kagunguli, Makamu wa Rais aliwapa pole wananchi wa kisiwa hicho baada ya kukumbwa na tufani ya kimbunga cha upepo iliyotokea tarehe 04 Novemba 2016 na kusababisha uharibifu mkubwa ikiwemo nyumba za watu kubomoka.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages