Hospitali Ya Taifa Muhimbili Yapokea Msaada Wa Mashine Kubwa Ya Utrasound Yenye Uwezo Mkubwa Wa Kung’amua Magonjwa Ya Figo.

Hospitali Ya Taifa Muhimbili Yapokea Msaada Wa Mashine Kubwa Ya Utrasound Yenye Uwezo Mkubwa Wa Kung’amua Magonjwa Ya Figo.

Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea  msaada wa mashine kubwa na ya kisasa  ya Utra Sound maalum  kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya Figo.

Msaada huo umetolewa  jana na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha nchini Norway ambapo pamoja na mambo mengine wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano  katika maeneo ya elimu , utafiti pamoja na vifaa tiba.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo ambaye pia Mhadhiri kutoka MUHAS Paschal Ruggajo  amesema mashine hiyo itasaidia kuchukua sampuli ya figo kwa ajili ya kugundua  magonjwa  ya Figo , kuweka vifaa kwenye mishipa damu kwa wagonjwa wanaoanzishiwa matibabu ya uchujaji wa damu na kugundua matatizo mbalimbali ya Figo.

“ Kwa muda mrefu sasa tumekua na ushirikiano wa karibu kati ya Hospitali hiyo , MUHAS na MNH  na wametusaidia kufundisha Madaktari sita wa Figo , wameshatoa mashine za kusafisha Figo na sasa wametupatia mashine hii kubwa ya Utra Sound kwakweli tunawashukuru kwa msaada wao.” Amesema Dk. Ruggajo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Dk . Hedwiga Swai ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba ameishukuru Hospitali hiyo ya Haukeland  na kusisitiza kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka kwakua  mashine hiyo itasaidia sana katika kitengo cha Figo
Profesa Einar Svastard ( kulia)   akimkabidhi  msaada wa mashine kubwa ya kisasa ya Utrasound  Mkurugenzi wa huduma za tiba  MNH Dk. Hedwiga Swai  .
Profesa Einar Svastard akimfanyia uchunguzi mgonjwa kwa kutumia mashine hiyo
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages