Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wengine watatu

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wengine watatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa wenyeviti wawili wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii na mmoja wa chuo.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi iliwataja walioteuliwa kuwa ni kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Alhaji Mussa Iyombe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Mhandisi Alhaji Mussa Iyombe ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Pili, Rais Magufuli amemteua Prof. Faustine Karani Bee kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF)

Prof. Faustine Karani Bee ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Prof. Tadeo Andrew Satta kuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Kabla ya uteuzi huu Prof. Tadeo Andrew Satta alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages