Kifo cha Lech Kaczynski kuchunguzwa
Waendesha mashtaka w nchini Poland wameanza kuuchunguza mwili wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo,Lech Kaczynski, na mkewe ikiwa ni sehemu ya uchunguzi mpya wa ajali ya ndege ambayo ilisababisha vifo vyao.
Kesi hiyo imefunguliwa upya na Chama cha Poland kinachosimamia Sheria na Haki , ambacho kinaongozwa na kaka wa Kaczynski, Bwana Jaroslaw. Serikali ya Poland inaamini kwamba ndege hiyo imeangushwa kusudi kwa bomu, na sio hali mbaya ya hewa au makosa ya rubani kama uchunguzi wa awali ulivyobaini.
Ndege hiyo ilipata ajali mwaka 2010 wakati ilipokuwa imewabeba viongozi wakuu kutoka nchini Urusi.
No comments:
Post a Comment