Maandamano ya kumpinga rais wa Korea Kusini yafanyika Seoul
Maelfu ya raia wa Korea Kusini wamekusanyika kati kati mwa mji wa Seoul kufanya maandamao ya kumpinga Rais Park Geun-hye.
Wengi wanataka ajiuzulu kufuatia madai kuwa alimruhusu rafiki wake wa muda mrefu, kuwa na ushawishi kwenye masuala ya serikali.
Siku ya Ijumaa rais alitoa hotuba kwa njia ya televisheni akisema kuwa kashfa hiyo ilitokana na makosa yake.
Bi Park alijipata chini ya ushawishi wa mwanamke kwa jina Choi Soon-sil ambaye kwa sasa yuko kuzuizini.
Bi Choi anadaiwa kutumia fursa yake kunufaika kifedha
No comments:
Post a Comment