Maombi ya dhamana ya Godbless Lema kuwasilishwa leo Baada ya Jana Kushindikana

Maombi ya dhamana ya Godbless Lema kuwasilishwa leo Baada ya Jana Kushindikana

Mawakili wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambaye yupo mahabusu katika Gereza kuu la Kisongo, jana walishindwa kukamilisha taratibu za kisheria za kuwasilisha maombi ya dhamana Mahakama Kuu .

Wakili wa Lema, John Mallya jana alisema watawasilisha maombi hayo leo wakati wa kusikilizwa kesi nyingine za mteja wao. “Bado kuna taratibu zinaendelea na tunatarajia kesho (leo) tutazikamilisha,” alisema Mallya. 

Katibu wa Mbunge Lema, Innocent Kisayegi, alisema baadhi ya mawakili wa Lema walikuwa na kikao cha kisheria kujipanga kwa kesi ya leo huku wakisubiri timu nyingine ya mawakili kutoka makao makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam. 

“Muda huu leo (jana) mawakili wanaendelea na kikao na tuna imani leo watakuwa tayari kwa utetezi wa Lema,” alisema. 

Mawakili wa Lema ambao jana walikutana ni James Lyatuu, Sheck Mfinanga na Charles Aidieli na wanatarajia kuungana na mawakili wengine akiwamo Mallya. 

Hata hivyo, Kisayegi aliwataka wakazi wa Arusha wajitokeze mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili mbunge huyo na mkewe. 

Lema anakabiliwa na mashtaka ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli ambayo yanatajwa kusababisha kukosa dhamana kutokana na rufani ya dhamana yake kuwekewa pingamizi na wanasheria wa Serikali. 

Lema na mke wake, pia wanakabiliwa na kesi ya kutuma ujumbe wa uchochezi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na shitaka jingine la kuhamasisha maandamano ya Ukuta Agosti.
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages