Home »
» PLUIJM – MBEYA CITY WALICHEZA VEMA DHIDI YETU

Pluijm alisema kuwa bao la pili katika mchezo huo halikustahili kwani maamuzi yake yalikuwa na utata na kwamba aliwaamuru wachezaji wake warudi nyuma kabla ya filimbi kupigwa na Mbeya City wakatumia mwanya huo kufunga.
“Mbeya City ni timu nzuri, wana uwezo wa kucheza dakika 90 bila kuchoka na timu ndio inavyotakiwa kuwa, lakini mwamuzi hakuwa makini, amewaumiza wachezaji wangu kiakili na kuwatoa mchezoni, aliwasababisha wacheze chini ya kiwango,” alisema Pluijm ambaye amedai kuwa anajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Prisons.
“Naweza kusema ilikuwa ni siku mbaya kwetu, wachezaji wangu wameniangusha hawakucheza soka ninalolihitaji, hata hivyo, natumaini mchezo ujao tutacheza vizuri,” alisema.
Kwa matokeo hayo, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wanabaki na pointi zao 27 wakiwa wamecheza mechi 13 wakiwa nyuma ya pointi nane dhidi ya mahasimu wao Simba ambao wana pointi 35 wakicheza michezo 13 sawa na Yanga.
No comments:
Post a Comment