Uingereza: Vikwazo vya mahakama havitazuia kujiondoa EU
Msemaji wa serikali ya Uingereza amesema vikwazo vya mahakamani havitoharibu mipango yake ya kuanza rasmi mchakato wa kujiondoa katika umoja wa ulaya mwishoni mwa Machi.
Serikali inasema itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya juu kwamba lazima ipate uungwaji mkono wa bunge kabla kuanza rasmi kipengele cha kujitoa.
Wote walioleta kesi wamehoji kuwa serikali haiwezi kutumia mamlaka hii kukwepa bunge na kuondoa haki ya kiseria.
Mahakama ya juu inatarajiwa kusikiliza rufaa mwezi ujao.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya sheria anaelezea jambo hili kuwa linaweza kupelekea mgogoro mkubwa wa kikatiba.
No comments:
Post a Comment