AI: Kenya inawalazimisha wakimbizi kurudi Somalia
Shirika la kupigania haki za kibinaadamu la Amnesty International limeishtumu serikali ya Kenya kwa kuwalazimisha wakimbizi wa Somalia kurudi makwao.
Amnesty International inasema kuwa maafisa wameambia raia hao katika kambi ya Dadaab ambayo inawahifadhi zaidi ya wakimbiizi 250,000 ,kwamba watalazimishwa kuondoka iwapo hawatakuwa wameondoka kufikia mwisho wa mwezi.
Kundi hilo limeushtumu Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kwa kushindwa kuangazia hatari itayowakabili raia hao nchini Somalia.
Lakini msemaji wa serikali Erick Kiraithe ameambia BBC kwamba shutuma hizo sio za kweli.
''Tumeona baadhi yao wakikataa lakini wengi wa wakimbizi wamekubali kwamba wanafaa kuanza maisha mapya,na wako tayari kuondoka'', alisema.Sio serikali inayowalazimisha kuondoka.
Walipoelezwa kuhusu vile watakavyorudi nchini mwao waliona ni bora''.
Mawaziri wa serikali ya Kenya wametoa ishara zisizoeleweka kuhusu iwapo kambi hiyo itafungwa kama ilivyopangwa.
No comments:
Post a Comment