Kesi ya Godbless Lema na mkewe kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha yakwama kusikilizwa..

Kesi ya Godbless Lema na mkewe kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha yakwama kusikilizwa..

Kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless lema na mke wake Neema Lema (33), imeshindwa kusikilizwa maelezo ya awali.

Hatua hiyo ni baada ya Mbunge huyo kukwama kuletwa Mahakamani toka Mahabusu kwa sababu zisizojulikana.

Kukosekana kwa Mbunge huyo kuonekana Mahakamani, kulimlazimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Agustino Rwezile kutoa amri ya kutolewa hati ya kumtoa Mahabusu mshitakiwa huyo na kumleta mahakamani hapo ili kesi hiyo isikilizwe maelezo ya awali.

Hata hivyo tangu amri hiyo itolewe saa nne asubuhi hadi saa saba mchana mshitakiwa hakuweza kuletwa mahakamani hapo, licha ya mke wake kuwepo mahakamani hapo.

Rwezile alimtaka wakili wa serikali kueleza sababu za kushindwa kumleta Lema Mahakamani wakati Mahakama imetoa amri.

Wakili wa serikali Fotunatus Mhalila alisema mshitakiwa ameshindwa kuletwa Mahakamani kutokana na sababu zisizozuilika , ila kwa sababu upelelezi umekamilika aliomba Mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa hoja za awali.

Majibu hayo yalipingwa vikali na Wakili wa utetezi, John Mallya ambaye alitaka kufahamu sababu za kutomleta Lema anazodai hazikuweza kuzuilika ni zipi na kwa nini zisitajwe  mahakamani. 

“Mheshimia hakimu hizo sababu zisizoweza kuzuilika ni zipi, Wakili wa seriali atueleze, tujue kama siyo amedharau mahakama licha ya kutakiwa kumleta mshitakiwa,” alisema.

Baada ya hoja hizo kutolewa Hakimu Rwezile aliendelea kusisitiza hati ya kumtoa Mahabusu itolewe ili aletwe Mahakamani leo katika kesi hiyo, ambayo itasikilizwa hoja za awali.

Awali katika kesi hiyo Godbless Lema na mke wake Neema, alisomewa mahitaka kuwa kati ya Agosti 20 Mwaka huu ndani ya Arusha,walimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani Mkuu huyo wenye lugha ya matusi , huku wakijua ni kosa kisheria. 

Ilidaiwa kuwa ujumbe huo ulitumwa kutoka 076415**47 namba 075655**18 kwenda namba 0766-75**75 ukidai, “Karibu, tutakuthibiti kama Uarabuni wanavyothibiti mashoga.” Washitakiwa walikana shitaka hilo na walipatiwa dhamana
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages