Lipumba Atishia Kumpiga Marufuku Maalim Seif Kufanya Mikutano Tanzania Bara

Lipumba Atishia Kumpiga Marufuku Maalim Seif Kufanya Mikutano Tanzania Bara

Mwenyekiti    wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema atampiga marufuku Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kufanya mikutano ya kisiasa Tanzania Bara kama hatamtambua kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho.

Lipumba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na viongozi wa CUF kwenye mkutano wa ndani mkoani Geita.

Ziara ya Lipumba imefanyika wakati Maalim Seif akiwa amesambaza barua kwa viongozi wa CUF wa wilaya zote nchini akiwataka wasishirikiane na Profesa Lipumba huku akionya atakayekaidi atachukuliwa hatua.

“Kama Maalim Seif hatambui kuwa mimi ni mwenyekiti wake, huku mimi nikimtambua kuwa Katibu Mkuu wangu, basi naye tutamzuia kufanya mikutano ya kisiasa Tanzania Bara,” alisema Lipumba.

Profesa Lipumba alisema hana tatizo na wananchi wa Zanzibar wala kiongozi wa upinzani atakayetetea watu hao na kuongeza kuwa yeye amekuwa mstari wa mbele kutetea Wazanzibari.

“Mimi natambua kuwa ndiye mwenyekiti halali wa chama hiki na mwenye mamlaka ya kumwondoa mwenyekiti au katibu ni mkutano mkuu wa chama na lazima theluthi moja ya wajumbe watoke Bara na theluthi nyingine Zanzibar, lakini mkutano huo haukufanyika wala muhtasari haupo,” alisema Profesa Lipumba.

Alieleza kwamba kwa sasa yeye na wana CUF wengine wamejipanga kukijenga chama hicho.

Mwenyekiti huyo pia alizungumzia suala la Muungano akisema ni muhimu kwa usalama wa nchi na Taifa kwa ujumla.

Alisema ili kulinda Muungano kuna mahitaji muhimu ya kuwa na vyama vyenye nguvu vitakavyokuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wananchi wa pande hizo mbili.

Lipumba alisema amefika wilayani hapa akitoka Urambo kwenye msiba wa Spika wa Bunge la Tisa, marehemu Samuel Sitta ambapo pia aliongea na baadhi ya viongozi wa chama hicho.

“Tumeifika Kahama kuzungumza na viongozi wa hapa na wa wilaya jirani, dunia ina changamoto kubwa katika masuala ya demokrasia na kujenga utawala bora kwa baadhi ya viongozi,” alisema Lipumba.
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages