Maelfu waandamana kupinga ushindi wa Trump Marekani

Maelfu waandamana kupinga ushindi wa Trump Marekani


Mwandamanaji San franciscoImage copyrightREUTERS
Image captionBaadhi wamebeba mabango yanayosema "Not my president" (Si Rais wangu)
Maelfu ya watu wameandamana katika miji mbalimbali nchini Marekani kupinga ushindi wa Donald Trump wa chama cha Republican.
Wengi wamekusanyika nje ya jumba maarufu la rais huyo mteule Trump Tower mjini New York wakipaza sauti zao dhidi ya msimamo wa Bw Trump kuhusu sera za uhamiaji, mapenzi ya jinsia moja na haki ya uzazi yanayopingwa na Donald Trump.
Wanasema hata dunia ina wasiwasi juu ya ushindi wake.
Wameandamana licha ya Rais Obama kuhimiza umoja na Bi Clinton kuwaambia wafuasi wake kwamba Bw Trump anafaa kupewa "nafasi ya kuongoza".
Rais Obama anatarajiwa kukutana na Bw Trump baadaye leo katika ikulu ya White House ambapo watajadiliana kuhusu shughuli ya mpito na kupokezana madaraka.
Mamia ya waandamanaji wanaompinga Trump walikusanyika nje ya jumba kuu la Bw Trump, Trump Tower eneo la Manhattan jijini New York Jumatano jioni, wakibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe "Not my president" (Si Rais wangu), pamoja na mabango mengine.
Polisi hapo awali waliweka vizuizi vya saruji pamoja na kuchukua hatua nyingine za kiusalama nje ya jumba hilo refu linalopatikana barabara ya 5th Avenue, jumba ambalo huenda likawa makao makuu ya Bw Trump wakati wa kipindi cha mpito kabla yake kuingia White House.
Trump Tower, New YorkImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionPolisi wameweka vizuizi vya Trump Tower
Kuliripotiwa pia taarifa za waandamanaji kuziba lango la kuingia jumba la Trump Tower mjini Chicago Jumatano jioni, wakiimba: "No Trump, No KKK, No Fascists USA" (Hatumtaki Trump, Hatutaki KKK, Hatutaki Wafashi Marekani) na "Not my president!" (Si Rais wangu).
Mjini Oakland, California, na Portland, Oregon, waandamanaji waliteketeza bendera za Marekani.
Wakati wa hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi mapema Jumatano, Bw Trump aliahidi kuponya vidonda vya migawanyiko, baada ya uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali, na kuahidi kwamba atakuwa "rais wa Wamarekani wote".
Msemaji wa White House Josh Earnest amesisitiza kwamba Bw Obama atakuwa na uwazi kuhusu kuhakikisha shughuli laini ya mpito atakapokutana na Bw Trump, ingawa aliongeza kwamba: "Sijasema kwamba utakuwa mkutano rahisi."
Waandamanaji ChicagoImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionWaandamanaji nje ya Trump Tower mjini Chicago
Rais huyo mteule atasindikizwa kwenda White House Alhamisi na mkewe, Melania, ambaye atakutana na Mke wa Obama, Michelle.
Kinyago cha Trump Los AngelesImage copyrightREUTERS
Image captionMjini Los Angeles waandamanaji waliunda kinyago kinachofanana na Trump...
Kinyago cha Trump mjini Los AngelesImage copyrightREUTERS
Image caption... na baadaye wakakichoma.
Wanafunzi wa shule ya upili ya Berkeley wakiandamana kupinga ushindi wa TrumpImage copyrightREUTERS
Image captionWanafunzi wa shule ya upili ya Berkeley wakiandamana kupinga ushindi wa Trump
Bw Obama, aliyempongeza mrithi huyo wake kwa njia ya simu mapema Jumatano, alisema si siri kwamba yeye na Bw Trump wana tofauti nyingi.
Lakini aliongeza kwamba wanataka kuhakikisha wanalinda maslahi ya taifa na kwamba alitiwa moyo na yale Bw Trump alikuwa amesema usiku uliotangulia.
Kundi la kushughulikia shughuli ya mpito la Bw Trump litaongozwa na Chris Christie, gavana wa New Jersey, na lina wiki 10 kukamilisha maandalizi hayo.
San franciscoImage copyrightREUTERS
Image captionWengi wameshangazwa na ushindi wa Trump
Rais huyo mteule, ambaye hajawahi kuhudumu katika wadhifa wowote wa kuchaguliwa au kuteuliwa serikalini, amesema kipaumbele chake kitakuwa kufufua na kuimarisha miundo mbinu ya nchi hiyo pamoja na kukuza ukuaji wa uchumi wa taifa hilo maradufu.
Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha Republican Reince Priebus alisema: "Donald Trump anachukulia hili kwa uzito sana," na kuongeza kwamba mfanya biashara huyo tajiri atatumia uwezo wake wa kutetea na kufanikisha mikataba ya kibiashara kuhakikisha mambo mema "yanatendeka kwa Wamarekani" haraka iwezekanavyo.
Trump Tower, New YorkImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionMwandamanaji mwenye bango nje ya jumba la Trump Tower, New York
Waandamanaji CaliforniaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionWaandamanaji California
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages