Marekani yalazwa 4-0 na Costa Rica mechi ya kufuzu Kombe la Dunia
Marekani imepata kipigo kikali katika mechi za kufuzu kwa kombe la dunia kwa miaka 36 baada ya kupokea kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Costa Rica siku ya Jumanne.
Mshambuliaji Joel Campbell alifunga mabao mawili kwa wenyeji hao, huku Johan Venegas na Christian Bolanos wakaongeza mabao mawili.
Meneja wa Marekani Jurgen Klinsmann, ambaye upande wake ulipoteza katika mechi yao ya kwanza, amesema 'ni pigo ambalo lina uchungu zaidi' kwa miaka yake mitano ya huduma kama meneja.
''Ni wakati wenye uchungu kwetu sisi. Hatuna shaka kuhusiana na hilo,'' alisema Klinsmann
Marekani haijawahi kupoteza kwa mabao manne tangu mwaka wa 1980 walipochapwa mabao 5-1 na Mexico.
Kwa hivi sasa wako katika nafasi ya mwisho kati ya nchi sita zilizofuzu katika hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment