Pistorius ahamishiwa gereza lenye vifaa bora
Mamlaka ya magereza nchini Afrika Kusini imemhamisha mwanariadha mlemavu wa nchi hiyo Oscar Pistorius, kwenda gereza lenye vifaa bora kwa watu walemavu.
Mwanariadha huyo wa zamani anayetumikia kifungo cha miezi sita jela kwa kumuua mpezi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013, amehamishwa kwenda kituo cha kurekebisha tabia cha Atteridgeville, ambacho kilifanyiwa ukarabati kuwafaa watu walemavu.
Awali alikuwa amefungwa katika gereza la Kgosi Mampuru II.
Idara ya vituo vya kurekebisha tabia inasema Atteridgeville, kinawahifadhi wafungwa wenye vifungo visivyozidi miaka 6 na kina programu za kurekebisha tabia kwa wafungwa.
Waendesha mashtaka wamekata rufaa kupinga kifungo cha Pistorius wakidai kuwa ni kifupi mno.
Mshindi huyo mara sita wa dhahabu katika mashindano ya walemavu aliandikisha historia kwa kuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kushiriki mashindano ya olimpiki mwaka 2012 mjini London akitumia miguu bandia.
No comments:
Post a Comment