Trump aimarika huku Clinton akiendelea na kampeni
Huku kura ya maoni ikionyesha kuwa Donald Trump anaendelea kupata uungwaji mkono, Hillary Clinton naye amekuwa akifanya mikutano katika majimbo ambayo yameonekana kuwa ngome ya chama cha Democratic.
Kwa sasa pande zote zinafanya mikakati ya kuwashauri wapigaji kura kupiga kura baada ya kuwarai wale ambao bado hawajafanya uamuzia.
Inadhaniwa kuwa zaidi ya watu milioni 37 tayari wamepiga kura.
Huku ikiwa zimebakia siku tatu pekee kabla ya upigaji kura mawakili wa chama cha Democratic wameanza kuwasilisha kesi mahakamani wakisema maajenti wa Donald Trump wameanza mtindo wa kuhakikisha kuwa watu fulani hawapigi kura siku ya upigaji kura.
Bwana Trump ametoa wito kwa mawakili wake watekeleze wajibu wa wachunguzi ili kujiepusha na ulaghai na hali ambapo mtu haibi kura.
Katika jimbo la Ohio, Jaji ametoa amri dhidi ya kundi la kampeni la Donald Trump lihakikishe kuwa halishiriki katika kuwatisha watu wanaotaka kupiga kura.
Wakati huohuo Bi Clinton ameungana na mwanamziki wa mtindo wa Rap, Jay Zee katika hafula maalumu inayokusudia kuwarai wapiga kura wenye asili ya Afrika wajitokeze kwa wingi Jumanne kupiga kura.
Kura ya maoni ya sasa inaonyesha kuwa kura yoyote itakayopigwa itatekeleza wajibu muhimu kuamua ni nani atakayeongoza.
Inaonekana kuwa Donald Trump amekaribiana sana na Bi Clinton na hakuna uhakika kuwa ni nani atakayeshindwa kwa wakati huu.
No comments:
Post a Comment