Watoa huduma za misaada 20 watekwa Sudan Kusini
Wafanyakazi ishirini wa kutoa misaada wametekwa nyara katika mji wa Nhialdiu nchini Sudan Kusini baada ya mji huo kudhibitiwa kwa muda na vikosi watiifu kwa makamu wa rais aliyefutwa Riek Machar katika jimbo la Liech Kaskazini.
Waziri wa habari nchini Sudan Kusini Lam Tungwar Kueigwong, alisema kuwa hatua zinachukuliwa kuwarudisha watoa misaada hao lakini hakutoa taarifa za kina.
"Hiki ni kisa kibaya kwa hali ya kibinadamu na watu wa Liech Kaskazini kwa ujumla," waziri alinukuliwa akisema.
Mzozo uliibuka mwaka 2013 ba\da ya rais Salva Kiir, kumlaumu bwana Machar kwa kupanga mapinduzi, madai ambayo Machar aliyakanusha.
No comments:
Post a Comment