BOT Yasitisha Kuweka Dhahabu Kama Hazina Ya Rasilimali Za Kigeni

BOT Yasitisha Kuweka Dhahabu Kama Hazina Ya Rasilimali Za Kigeni


Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesitisha kuweka dhahabu kama hazina ya rasilimali za kigeni kwa sababu ya kuyumba kwa bei ya madini hayo katika soko la dunia na kusababisha uwezekano wa kupunguza thamani ya hazina ya rasilimali ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga Mhe. Dalaly Kafumu aliyehitaji kufahamu sababu za Serikali kukataa kutunza dhahabu safi katika Benki Kuu wakati Tanzania ni nchi mojawapo inayozalisha dhahabu safi.

Mhe. Kijaji alisema kuwa jukumu la msingi la Benki Kuu ni kuandaa na kutekeleza Sera ya Fedha inayolenga kuwa na utulivu wa bei kwa ajili ya ukuaji endelevu wa uchumi wa Taifa hivyo ili kufanikisha azma hiyo Benki Kuu inadhibiti ongezeko la ujazi wa fedha kwa kutumia nyenzo mbalimbali zikiwemo za kuuza dhamana na hati fungani za Serikali pamoja na kushiriki katika soko la jumla la fedha za kigeni kati ya mabenki.

“Katika kutekeleza jukumu lake la msingi, Benki Kuu hutunza hazina ya rasilimali za kigeni zinazotosha kuagiza bidhaa nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne lakini kwa muda mrefu sasa Benki Kuu ya Tanzania haiweki dhahabu kama sehemu ya rasilimali hizo kutokana na kuyumba kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia”, alisema Mhe. Kijaji.

Naibu Waziri huyo alitoa mfano wa kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la Dunia ambapo dhahabu ilishuka kutoka dola 1,745 za kimarekani katika mwezi Septemba 2012 hadi dola za kimarekani 1,068 kufikia mwezi Desemba 2015.

Mhe. Kijaji alifafanua kuwa hazina ya rasilimali za kigeni zinaweza kuwa dhahabu – fedha (monetary gold) au fedha za kigeni ambapo uamuzi kuhusu hazina itunzwe vipi unazingatia vigezo mbalimbali vikiwemo vile vya kudumisha thamani, wepesi wa kubadilisha pamoja na faida inayopatikana kwa kuwekeza hazina hiyo.

Aidha, Mhe. Kijazi alisema kuwa ununuzi na uuzaji wa madini ya dhahabu unahitaji ujuzi maalum ambapo kwa kuzingatia jukumu la msingi la Benki Kuu inaonyesha dhahiri kuwa Benki hiyo haijajijengea uwezo katika eneo la biashara ya madini hayo.
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages