Malema afika mahakamani kujibu mashtaka ya uchochezi
Mwanasiasa wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema, amefika mahakamani kwa mashtaka ya kuwachochea watu akiwataka kunyakua mashamba yanayomilikiwa na wazungu.
Hata hivyo kesi hiyo ilihairishwa hadi mwezi Juni mwaka ujao kumpa Malema muda wa kupinga kipengee cha katiba kilichotumiwa enzi ubaguzi wa rangi kumshtaki.
Malema alifika katika mahakama ya mji wa Bloemfontein kutokana na hotuba aliyotoa mwaka 2014, ambapo alisema:
"Tutainyakua ardhi ambayo hayajakaliwa kwa sababu tuniataka ardhi hiyo. Ili sisi tule ni lazima tuinyakue ardhi hiyo. Ili sisi tufanye kazi ni lazima tuinyakue...Ninatoka Seshego. Kama kuna ardhi yenye haina watu eneo langu , nataenda niinyakue. Ni lazima uende ufanye hivyo hivyo katika eneo unatoka"
Malema alifika mahakama nyingine kwa mashtaka kama hayo wiki iliyopita, kufuatia hotuba aliyotoa mwezi Juni ambapo alisema kuwa wazungu hawastali kudai kuwa wanamiliki ardhi, kwa sababu ilikwa ni ya watu weusi ambao ndio wengi nchini humo.
No comments:
Post a Comment