Raia wa Nigeria aliyekutwa na bangi kunyongwa Singapore

Raia wa Nigeria aliyekutwa na bangi kunyongwa Singapore


Walanguzi wa dawa za kulevya huhukumiwa kifo SingaporeImage copyrightAFP
Image captionWalanguzi wa dawa za kulevya huhukumiwa kifo Singapore
Singapore imekataa ombi la msamaha kutoka kwa raia mmoja wa Nigeria ambaye amepangiwa kunyongwa Ijumaa kwa kupatikana na bangi, shirika la haki za kibinadamu la Amnesty International limesema.
Familia ya Chijoke Stephen Obioha ilifahamishwa kuhusu hatua hiyo Jumatano.
Obioha alipatikana na kilo 2.6 za bangi Aprili 2007, kiasi kilichokuwa kimezidi kipimo cha gramu 500 ambacho mara moja humfanya mtu kuhukumiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya chini ya sheria za Singapore.
Afisa wa Amnesty International Rafendi Djamin amesema shirika hilo limeshangazwa na hatua hiyo ya Singapore kumnyima mshtakiwa huyo msamaha.
Hata hivyo, alisema shirika hilo bado lina matumaini kwamba Singapore haitatekeleza adhabu hiyo "katili na isiyoweza kubatilishwa dhidi ya mtu huyo aliyehukumiwa kifo kwa kosa ambalo halifai adhabu ya kifo."
"Hukumu ya kifo si suluhu. Haitaangamiza daw azote za kulevya Singapore. Kwa kuwanyonga watu kwa makosa ya kuwa na dawa za kulevya, ambayo hayafikii kiwango cha makosa makubwa ya uhalifu, Singapore inakiuka sheria za kimataifa.
"Mataifa mengi ulimwenguni yameacha adhabu hii ya kikatili, kinyama nay a kudunisha."
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages