Uganda yawashinda Congo Brazzaville bao 1-0
Uganda imejizolea pointi nne katika kundi E kwenye mechi za kufuzu kwa kombe la dunia kwa kuwatandika Congo Brazzaville bao 1- 0.
Bao hilo lililofungwa na mshambuliaji Farouk Miya mnamo dakika ya 18 liliwaweka Crane Uongozini na kuwapandisha katika jedwali hadi namba moja katika kundi lao.
Miya ambaye huijizea Standard Liege nchini Ubelgiji alidhibiti mpira na kuvurumisha kombora kali lililomchanganya kipa wa Congo Brazzavile Mongondza Ngobo.
Kwngineko Afrika kusini iliwashinda Senegal kwa mabao 2-1 na kuingia kilele mwa kundi D.
Hii nido mara ya kwanza Senegal inashindwa tangu ipoteze kwa Algeria wakati wa mechi za makundi kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment