IMF kuipa Misri mkopo wa dola bilioni 12
Shirika la fedha duniani IMF limeidhinisha mkopo wa miaka mitatu wa dola bilioni 12 kwa taifa la Misri ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na hali ngumu ya uchumi.
Misri itapokea dola bilioni 2.75 mara moja, huku zingine zikifuatia kulingana na vile itaimarika kiuchumi na kufanya mabadiliko.
Mkurugenzi wa IMF Christine Lagarde, anasema kuwa mkopo huo utatumiwa kukabiliana na changamoto nyingi.
Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi anakabiliwa na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira na upungufu wa bajeti wa asilimia 12.
Nchi hiyo imepata wakati mgumu kuvutia wawekezaji wa kigeni tangu ikumbwe na mzozo wa kisiasa mwaka 2011, ambao ulisababisha Rais Hosni Mubarak kuondolewa madarakani.
Utalii ambacho ndicho kitega uchumi muhimu cha nchi hiyo, umedidimia mwa kipindi cha miaka mitano.
Wiki iliyopita serikali iliongeza riba ya mikopo kwa asilimia 3 hasi asilimia 14.75 na pia kuongeza bei ya bidhaa muhimu na mafuta.
Hatua hizo zilisababisha rais kukoselewa vikali na kushuka kwa umaarufu wake.
No comments:
Post a Comment