Watu 17 wauawa kwenye mlipuko Iraq
Polisi wa Iraq wanasema kuwa watu 17 wameuwawa, katika milipuko ya mabomu yaliyotegwa kando ya barabara, wakati walikuwa wakiwakimbia wapiganaji wa Islamic State, Kaskazini mwa nchi.
Milipuko miwili ilipiga lori, lilobeba familia zilizokuwa zikiukimbia mji wa Hawija, unaodhibitiwa na kundi la Islamic State.
Polisi kwenye gari jengine pia aliuwawa.
Jeshi la serikali ya Iraq linaendelea na operesheni kubwa ya kuukomboa mji wa Mosul, ulioko mikononi mwa Islamic State.
Pande hizo mbili zimekuwa zikirushiana mizinga na risasi, huku jeshi linajaribu kujizatiti katika mitaa iliyoikomboa, mashariki mwa Mosul.
No comments:
Post a Comment