MIROSLAV KLOSE atundika daruga.
Mfungaji bora wa muda wote kwenye michuano ya kombe la Dunia MIROSLAV KLOSE amestafu kucheza soka na sasa ataingia kwenye jopo la makocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani chini ya kocha mkuu JOACHIM LOW.
MIROSLAV KLOSE
Mfungaji bora wa muda wote kwenye michuano ya kombe la Dunia, MIROSLAV KLOSE amestafu kucheza soka na sasa ataingia kwenye jopo la makocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani chini ya kocha mkuu JOACHIM LOW.
Mshambuliaji huyo amecheza soka kwa miaka kumi na nane na anatundika daluga akiwa amefunga magoli kumi na sita kwenye michuano minne ya kombe la Dunia yaani ya 2002, 2006, 2010 na 2014 akifuatiwa na RONALDO DE LEMA mwenye magoli kumi na tano.
Pia MIROSLAV KLOSE ndiye mfungaji wa muda wote wa Ujerumani akiwa amefunga magoli 71 mbele ya LOTHAR MATTHAUS na mwenyewe amesema kwa sasa akiwa anastafu anafurahia mafanikio yake akiwa na timu ya Taifa na kuongeza kuwa maisha yalikuwa mazuri mno enzi anacheza soka na hawezi kuyausahau maisha hayo.
MIROSLAV KLOSE anastafu soka akiwa ametwaa taji la bundersliga mara mbili,GERMAN CUP mara mbili,ubingwa wa Copa Italia akiwa na Lazio mara moja na kushika nafasi ya pili kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya. Mafanikio yake kwenye timu ya Taifa ni kutwa kombe la Dunia mara moja 2014 na mfungaji bora wa kombe la Dunia mara moja ilikuwa mwaka 2006.

No comments:
Post a Comment